Loading...
Rais wa Liberia George Weah amemshukuru kwa heshimu kubwa aliyekuwa kocha wa zamani wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger kwa kumpatia tuzo ya heshimu ya kusaka na kulea vipaji kwa wanasoka chipukizi wa Afrika.
"Umejitokeza kama mwalimu uliojitolea na kufanya mapinduzi ya muda wote kwa kusaka vipaji ulimwenguni kote, hasa barani Afrika," Alisema rais Weah kwa kocha wake wa zamani alipokuwa akiichezea Monaco ya Ufaransa, wakati wa sherehe hizo huko jijini Monrovia.
Maelfu ya watazamaji walifurahia wakati Wenga alipokuwa akitunukiwa medali ake katika ukumbi uliopo kwenye uwanja wa taifa.
Kocha mwingine, Claude Le Roy, ambaye alimwambia kwa mara ya kwanza kuhusu Weah, pia alitunukiwa tuzo hiyo.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WENGER ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA NA RAIS WEAH WA LIBERIA
Reviewed by By News Reporter
on
8/26/2018 01:42:00 PM
Rating:
![WENGER ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA NA RAIS WEAH WA LIBERIA](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhLnHs4I9jc7iXXovdEjcjE_H4C8gNOPB1wYnhA2uWb5zT0OrKQkMbMlP52GIQs6zYExf_KWltdxvnoWDmeXBLmuG_mXxw_RZVuYtEdgEO9oVHJ1Sexolu6l26P055iaGQQeEb0HqZ-1c/s72-c/wenger+and+weah.jpg)
Hakuna maoni: