Loading...

AUNTY LULU ADAI ANAJIPANGA KUMLOGA DIAMOND ILI AZAE NAE

Loading...
MSANII wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ametoa kali ya mwaka baada ya kueleza kuwa licha ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni kusema kuwa amejifunza kuwa makini kwa kutumia kinga ili asiendelee kupata watoto wa nje ya ndoa ‘side kid’, mwanadada huyo ameapa kuwa atamloga mpaka azae naye.

Akipiga stori na mtandao mmoja wa udaku, Aunty Lulu alisema ni ndoto yake ya muda mrefu kuzaa na Diamond hivyo ili itimie atafanya juu chini mpaka ampate hata kwa kumloga ili akikutana naye asahau hata kutumia kinga aweze kumpa ujauzito.

“Diamond amesema kwa sasa yuko makini ili asizae nje ya ndoa lakini kwangu mimi nitamloga mpaka aweze kuzaa nami kwa kuwa ni muda mrefu nina ndoto hiyo na hakuna kitakachonizuia maana namwamini sana mganga wangu,” alisema Aunty Lulu.
Na Lulu Frank.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
AUNTY LULU ADAI ANAJIPANGA KUMLOGA DIAMOND ILI AZAE NAE AUNTY LULU ADAI ANAJIPANGA KUMLOGA DIAMOND ILI AZAE NAE Reviewed by By News Reporter on 9/06/2018 12:21:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.