Loading...
Serikali ya Burundi yatishia kujiondoa katika jumuya ya mataifa ya Afrika Mashariki kutokana na matumizi ya lugha ya kiingereza katika taasi zake.
Pascal Nyabenda , msemaji wa bunge wa Burundi amefahamisha kuwa Burundi inaweza kujiondoa katika Jumuiya ya Mataifa ya Afrika Mashariki iwapo wito wake hautosikilizwa kuhusu matumizi ya lugha ya kiingereza.
Pascal amezungumza katika kituo cha redio ya taifa akirejea kutoka mjini Juba nchini Sudani Kusini ambapo alikuwa akishiriki katika mkutano wa wasemaji wa bunge wa mataifa ya jumuiya ya Afrika Mashariki amekemea njia zilizotumiwa katika uchaguzi wa msemaji wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Burundi inapinga matumizi ya lugha ya kiingereza kama moja ya vigezo vya kuajiri katika ofisi za jumuiya hiyo.
Kigezo hicho kinawaweka kando warundi kwa kuwa wao wanatumia lugha ya kifaransa.
Pascal Nyabenda amesema kuwa amefikisha malalamiko na kupendekeza lugha ya kifaransa kuwa lugha ya kazi pia katika jumuiya ya mataifa ya Afrika Mashariki.
Mataifa yanayojumuisha Jumuiya hiyo ni Burundi, Kenya, Uganda,Rwanda, Sudani Kusini na Tanzania.
Makao makuu ya jumuiya hiyo yapo mjini Arusha nchini Tanzania.
Na Leah Peter.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

BURUNDI YATISHIA KUJIONDOA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Reviewed by By News Reporter
on
9/24/2018 01:56:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: