Loading...

HUYU NDIYO MWANAMKE WA KWANZA KUTANGAZA HABARI SAUDI ARABIA

Loading...
Kwa mara ya kwanza nchini Saudi Arabia mwanamke ameonekana kutangaza habari katika runinga ya taifa.

Mtangazaji huyo wa habari  wa kike  aliwahi kufanya kazi katika jarida la Al-Hayat la mjini London, kituo cha runinga cha Al Jazeera na katika kituo cha runinga cha Al Arab.

Weam Al Dakheel aliajiriwa katika vituo hivyo baada ya kupata shahada yake ya uandishi wa habari katika chuo kikuu cha Marekani nchini Lebanon katika kitengo cha uandishi wa habari. 

Mwanamfalme wa Saudi Arabia ameahidi mabadiliko nchini humo kwa kuwapa uhuru wanawake.

Kwa sasa wanawake nchini Saudi Arabia wanaruhusiwa kuendesha magari na kuingia katika  kumbi za kuonesha filamu.
Na Mary Mkeu.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HUYU NDIYO MWANAMKE WA KWANZA KUTANGAZA HABARI SAUDI ARABIA HUYU NDIYO MWANAMKE WA KWANZA KUTANGAZA HABARI SAUDI ARABIA Reviewed by By News Reporter on 9/24/2018 01:33:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.