Loading...
Kununua vitu kwa bei nafuu ni njia moja wapo ya kuokoa pesa. Ikiwa unataka kununua nguo na ubane matumizi tembelea katika masoko haya.
Kuna masoko mengi jijini Dar es Salaam na baadhi yao ni maarufu kwa uuzwaji wa bidhaa fulani.
Kwa mfano, Soko la Tandale ni maarufu kwa uuzwaji wa nafaka, Mahakama ya Ndizi kama jina lake linavyojieleza ni maarufu kwa uuzwaji wa ndizi.
Mbali na masoko hayo, Ilala mchikichini maarufu kwa nguo za mtumba, Mwananyamala maarufu kwa nafaka pia.
Soko la Tandika
Sokoni Tandika ni soko ambalo linagonga vichwa vya watu wakati wanapofikiria kuhusu kununua nguo za mitumba. Hii haimaanishi kuwa hakuna nguo mpya za madukani. Soko la Tandika linakupatia nguo nzuri kwa bei nafuu.
Soko la Kariakoo
Soko la Kariakoo kwa mujibu wa Wikipedia linatambulika kama ni sehemu nzuri kununua nguo mbali mbali kama viatu, suruali, mashati, magauni n.k. Hili ni soko kubwa hapa Tanzania na Afrika Mashariki nzima.
Hapa pia utaweza kupata nguo kwa bei nafuu kwa wafanyabiashara maarufu kama machinga na madukani. Pia ndio soko ambali karibia kila kitu utapata na linalenga watu wa hadhi zote zakipato.
Soko la Ilala Mchikichini
Ni siku lililopo Ilala Mchikichini karibu na kiwanda cha TBL, maarufu sana kwa nguo za mtumba na mabatiki ya wakina mama. Sokoni humo utaweza kupata nguo za kila aina spesho na mtumba kwa bei nafuu sana.
Soko la Tandale
Soko la Tandale linapatikana katika manispaa ya Kinondoni, Tandale. Maarufu kwa nafaka lakini pia kuna nguo zote mtumba na spesho za bei rahisi ajabu mpaka kufika shati/flana kuuzwa mpaka Sh200/- kwa moja. Ni soko maarufu pia kwa watu wa hali ya chini kwa unafuu wa bei za nguo zake.
Soko la Buguruni
Soko maarufu kwa viungo na vyakula, linapatikana maeneo ya Buguruni karibu na Flyover ya Tazara. Katika soko hilo utapata nguo zote za mitumba na spesho kwa bei nafuu mno ujawahi kuona.
Na Neema Bushubo.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

MASOKO 5 UTAKAYONUNUA NGUO NA KUBANA MATUMIZI
Reviewed by By News Reporter
on
9/24/2018 01:26:00 PM
Rating:
Nimependa kuskia hili.
JibuFuta