Loading...

MKONGWE WA GOLF 'TIGER WOOD' ARUDI KWA KASI YA AJABU

Loading...
Mkongwe wa mchezo wa Golf, Tiger Woods amejinyakulia ushindi kwa mara ya kwanza tangu 2013 kwa kushinda mchezo muhimu katika michuano ya 2018 Tour Championship ikiwa ni msimu wa 80 kuhudhuria katika PGA tour.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 42, ambaye alikuwa majeruhi kabla ya kurudi mchezoni, alimshinda Billy Horschel katika mchezo wao uliofanyika katika uwanja wa East Lake Golf Club huko Atlanta siku ya Jumapili usiku.

Woods ambaye alishuka kiwango hadi kufikia nafasi ya 1,199 mwishoni mwa mwaka jana lakini anatarajiwa kupanda hadi nafasi ya 13 duniani baada ya ushindi huo wake wa kwanza kwa zaidi ya miaka mitano.

Tiger Woods anajulikana kwa umahiri katika mchezo huo wa golf kwa muda wote licha ya hivi karibuni kuonekana kushuka kiwango kutokana na majeruhi.
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MKONGWE WA GOLF 'TIGER WOOD' ARUDI KWA KASI YA AJABU MKONGWE WA GOLF 'TIGER WOOD' ARUDI KWA KASI YA AJABU Reviewed by By News Reporter on 9/24/2018 12:17:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.