Loading...

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI SUMATRA, KUFUATIA SAKATA LA MV NYERERE

Loading...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Mhandisi Dkt. John Ndunguru na kuivunja bodi hiyo kuanzia leo tarehe 24 Septemba, 2018.

Mhe. Rais Magufuli amechukua hatua hiyo kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba, 2018 na matukio mbalimbali ya ajali za barabarani hapa nchini yanayosababisha vifo, ulemavu na uharibifu wa mali.

Pamoja na hatua hiyo kamati ya uchunguzi ambayo itatangazwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa baadaye leo, itaendelea na uchunguzi wa ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kama ilivyopangwa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
24 Septemba, 2018
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI SUMATRA, KUFUATIA SAKATA LA MV NYERERE RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI SUMATRA, KUFUATIA SAKATA LA MV NYERERE Reviewed by By News Reporter on 9/24/2018 10:33:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.