Loading...
Kizaazaa kilizuka katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Narok, Kenya baada ya mwanaume mwenye umri wa miaka 28 kuzirai baada ya kupata habari kwamba mkewe amejifungua pacha watatu.
Kulingana na Francis Gitau, mkewe alikuwa tayari na pacha wengine wawili na alijawa na furaha baada ya kupokea pacha wengine watatu.
Gitau alisema kuwa licha ya kung'ang'ana kuwalea wale pacha wengine, alimshukuru Mungu kwa kumbariki kiwango hicho.
Akizungumza na wanahabari muda mchache baada ya kurudisha fahamu, Gitau alisema kuwa wasiwasi wake mkuu ni jinsi atakavyowalea watoto hao kwani gharama ya maisha imekuwa ghali kufuatia ongezeko la ushuru kwa bidhaa za mafuta ya petroli.
Kisa hiki kinafananishwa na kile cha jamaa mmoja aliyemtoroka mkewe kwa kujifungua pacha watatu na tayari alikuwa na pacha wengine wawili.
Mary Ng'anga alisema kuwa mumewe alimtoroka punde alivyopewa habari kwamba mkewe alikuwa amejifungua pacha watatu.
Inasemekana jamaa huyo hajulikani aliko kwa sasa na hata hapatikani kupitia njia ya simu.
Hata hivyo, Gitau na Mwihaki wamekubali jinsi hali ilivyo na wameahidiana kulea watoto hao kwa pamoja.
Na Bakari Juma.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

VISA NA MIKASA: JAMAA AZIMIA BAADA YA MKEWE KUJIFUNGUA PACHA WENGINE 3
Reviewed by By News Reporter
on
9/24/2018 10:14:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: