Loading...
Mabaharia 12 waliokuwa ndani ya meli ya Uswisi, waliotekwa na maharamia katika Bahari ya Atlantic Pwani mwa Nigeria, imebainika kuwa walikuwa wanatokea nchini Ufilipino, Slovenia, Ukraine, Romania na Bosnia.
Mabaharia hao walitekwa wakati meli yao ikitoka mjini Lagos kwenda mji mwingine wa Pwani wa Port Harcourt.
Utekaji nyara kama huu ni jambo la kawaida nchini Nigeria hasa katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta.
Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na kisa hiki, lakini na maharamia hao hawajazungumza chochote kuhusu mateka hawa, au kusem awanachotaka ili waweze kuachiliwa.
Kwa mujibu wa chanzo cha polisi nchini Nigeria, zoezi la kuwatafuta mabaharia hao linaendelea.
Na Hamisi Fakhi.Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
MAHARAMIA WA NIGERIA WATEKA MELI YA USWISI, MABAHARIA WATAMBULIWA
Reviewed by By News Reporter
on
9/24/2018 09:19:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: