Loading...

CHAMELEONE KUACHANA NA MKEWE UTATA MTUPU

Loading...
Msanii maarufu wa Afrika Mashariki Jose Chameleone aliwaacha wengi vinywa wazi baada ya kutangaza hadharani kuwa alikuwa ametengana na mkewe wa miaka mingi Daniella Atim.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, msanii huyo alieleza kuhusu jinsi alivyoamua kumtema mkewe akidai kuwa alikataa kumuamini kwa lolote.

Mkewe naye alijitokeza kuthibitisha msimamo wa mumewe kwa kuzifuta picha zote walizopiga pamoja katika kurasa zake za mitandaoni huku wengi wakihuzunika kuhusu kusambaratika kwa ndoa yao. 

Baadhi ya Mashabiki wake walidai kuwa hiyo ilikuwa kiki ya kutoa wimbo mpya na wala si kutalikiana.

Sasa imebainika kuwa msanii huyo hakutengana na mkewe ila ilikuwa kiki ya kutoa wimbo mpya. 

Hii ni baada ya msanii huyo kutambulisha wimbo wake mpya wa ‘Tatizo’, wimbo unaozungumzia changamoto katika ndoa. Hii ni baada ya msanii huyo kupost picha ya pamoja mtandaoni akiwa na mkewe huku wakionekana wakiwa wamependeza akiambatanisha picha hiyo na kauli ya kuthibitisha kuwa wamerudiana.

"Usiku mwanana wapendwa wangu Andreon Atim ❤Mungu azidi kutubarika pamoja na wanetu," Jose aliandika.

Ndoa kati ya Chemeleone na Atim imekumbwa na misukosuko huku mkewe akimlaumu msanii huyo huyo kwa ulevi na dhuluma.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
CHAMELEONE KUACHANA NA MKEWE UTATA MTUPU CHAMELEONE KUACHANA NA MKEWE UTATA MTUPU Reviewed by By News Reporter on 9/24/2018 09:00:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.