Loading...

HABARI ZA HIVI PUNDE: MBUNGE NAPE ANUSURIKA KIFO AJALINI

Loading...
Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Nape Moses Nnauye amenusurika kifo baada ya gari aina ya Land cruiser VX lenye namba 349 DEL alilokuwa amepanda kupinduka majira ya saa 1:00 asubuhi  ya leo, Jumatatu Septemba 24, 2018 katika Kijiji cha Kibutuka, wilaya Liwale, mkoani wakati akielekea Liwale kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dk.Bashiru Ali.

Imeelezwa kwamba, pamoja na Ziara ya Dkt. Bashiru, pia Nape alikuwa akienda Liwale kwa ajili ya kushiriki Kikao cha Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Lindi.

Nape alikuwa ameambatana na watu wengine wanne ambao wote ni wazima na hakuna mtu aliyedhurika lakini gari ndilo limeharibika kwa mbele. Mbunge Nachingwea, Masala amethibitisha.
Na Mohamedi Makame.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
HABARI ZA HIVI PUNDE: MBUNGE NAPE ANUSURIKA KIFO AJALINI HABARI ZA HIVI PUNDE: MBUNGE NAPE ANUSURIKA KIFO AJALINI Reviewed by By News Reporter on 9/24/2018 02:09:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.