Loading...

KENYA NA UGANDA WAENDELEZA MVUTANO UMILIKI WA KISIWA

Loading...
Huenda mvutano mkali ukaibuka tena kati ya Kenya na Uganda kuhusiana na umiliki wa kisiwa cha Migingo kilicho katika ziwa Victoria.

Hii ni baada ya serikali ya Uganda kushusha bendera ya Kenya iliokuwa katika kisiwa hicho na kutishia kwamba itakabiliana vilivyo na Kenya endapo bendera hiyo itarejeshwa.

"Waliondoa bendera ya Kenya kwenye kisiwa cha Migongo na kuwaonya maafisa wa polisi wa Kenya dhidi ya kuwachokoza," Mwenyekiti wa usimamizi wa kisiwa hicho John Obunge alisema.

Hata hivyo serikali ya Kenya imekimya tangu bendera hiyo iliposhushwa, ishara kwamba haitaki kujihusisha na vita vyovyote na serikali ya Uganda. 

Wavuvi wa kisiwa hicho waliikashifu serikali ya Museveni kwa kutowaheshimu raia wa Kenya wanaoishi karibu na kisiwa hicho.

Haya yanajiri mwezi mmoja tu baada ya waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i kuwaonya maafisa wa polisi wa Uganda dhidi aya kuwanyanyasa wavuvi wa Kenya.

"Tumebuni mpango wa kuwalinda watu wetu. Tutaweka usalama wa kutosha katika ziwa victoria, ni jambo la ghadhabisha kuwa mnyenyekevu na watu wanafikiria hauwezi ukafanya jambo lolote, tutakabiliana na wao vilivyo" Matiang'i alisema.
Na Paskali Joseph.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KENYA NA UGANDA WAENDELEZA MVUTANO UMILIKI WA KISIWA KENYA NA UGANDA WAENDELEZA MVUTANO UMILIKI WA KISIWA Reviewed by By News Reporter on 9/15/2018 08:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.