Loading...

KUNDI LA WANAFUNZI WANASWA WAKIFANYA NGONO

Loading...
Polisi mjini Bungoma, Kenya wamewanasa wanafunzi sita wa Shule za sekondari ambao wamekuwa wakiishi katika nyumba moja kwa kushiriki ngono kwa muda.

Kulingana na Chifu wa Bungoma Township Joseph Cheng’oli, wasichana hao wanne na wawili wa kiume walikamatwa Alhamisi, Septemba 13 na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Bungoma.

Chifu huyo alithibitisha kuwa wanafunzi hao walikuwa wamepanga nyumba karibu na shule moja katika eneo la bunge la Kandui walipokuwa wakiishi pamoja.

‘’ Wanafunzi hao wa Sekondari wenye umri wa miaka kati ya 14- 18 wamekuwa wakiishi pamoja kama wanandoa usiku, na mchana na ni wanafunzi katika shule moja,'' alisema.

"Tuliwakamata na kuueleza uongozi wa shule hiyo kuwaarifu wazazi wao ,’’ aliongezea. Aidha, alieleza kuwa wanafunzi hao watafikishwa hospitalini kwa vipimo. 

Chifu huyo alieleza kuwa alipewa habari kuhusu wanafunzi hao na wenyeji waliokuwa wamekerwa na tabia zao.

Afisa mmoja wa Nyumba Kumi aliuambia mtandao mmoja wa habari nchi humo kuwa baadhi ya wanafunzi hao walinaswa wakiwa uchi wa mnyama huku wengine wakinaswa wakiwa na chupi. 

‘’ Tuliwanasa walipokuwa wamepika na kumaliza kula, na walikuwa katika harakati ya kufanya tendo la ndoa. Tuliwakamata bila kutarajia huku tukivunja mlango wao na kuingia,’’ alisema.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KUNDI LA WANAFUNZI WANASWA WAKIFANYA NGONO KUNDI LA WANAFUNZI WANASWA WAKIFANYA NGONO Reviewed by By News Reporter on 9/15/2018 07:29:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.