Loading...

KOCHA PEP GUARDIOLA ATANGAZA NIA YA KURUDI HISPANIA

Loading...
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ametangaza wazi kwamba anataka kumalizia taaluma yake katika klabu ya Uhispania, Barcelona.

Raia huyo wa Uhispania aliye na umri wa miaka 47 alikuwa kocha wa Barcelona kati ya 2008 na 2012 ambako alishinda vikombe vingi.

Katika muda wa misimu miwili iliyopita, Pep Guardiola alijiunga na Manchester City akitokea Bayern Munich ya Ujerumani, lakini ilimbidi kungoja mpaka muhula wa pili kabla ya kushinda Premier League.

Akiongea na mchezaji wa zamani na meneja wa Real Madrid Jorge Valdano katika shoo yake, Universo Valdano, Pep Guardiola alisema analenga kurejea Barcelona.

''Nitamalizia kazi yangu nilipoanzia. Hatua zangu za mwisho zitakuwa katika klabu za ujanani wangu na ninatumainia kurejea Barcelona, ninaamini kumalizia na klabu bora zaidi,” aliema Pep Guardiola kulingana na ripoti iliyochapishwa na Daily Star UK.

Pep Guardiola aliongoza Barcelona mpaka ikawa miongoni mwa klabu bora zaidi La Liga, Copa del Rey na UEFA Champions League wakati wa msimu wake wa mwanzo Nou Camp. 

Mapema, iliripotiwa kuwa wachezaji wa Manchester City walipigwa marufuku na Guardiola kutumia simu za mkononi wakati wa mazoezi.
Na Julius Kishimba.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
KOCHA PEP GUARDIOLA ATANGAZA NIA YA KURUDI HISPANIA KOCHA PEP GUARDIOLA ATANGAZA NIA YA KURUDI HISPANIA Reviewed by By News Reporter on 9/15/2018 09:08:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.