Loading...
Kuna makazi huko Antaktika yenye shule, ofisi ya posta na msululu wa nyumba. Ni kama vijiji vingine vidogo, ila isipokuwa kitu kimoja tu: familia lazima zifanyiwe upasuaji ili kuishi mahali hapo.
Fikiria kwamba inabidi uondelewe 'kidole tumbo' ili uishi katika mji wako - na familia yako pia ifanye hivyo.
Hilo ndilo chaguo pekee lililopo kwa wakazi wa muda mrefu - hadi watoto lazima wafanye hivyo - wa Villas Las Estrellas, ikiwa ni moja ya makazi machache huko Antaktika ambapo watu wanaishi miaka mingi ukilinganisha miji ya jirani.
Kwanini kidole tumbo kinafanyiwa upasuaji na kinaondolewa?
Uondolewaji wa kidole tumbo ni tahadhari muhimu kwa wakazi hao wachache wanaoishi kijijini hapo kwa muda mrefu kwa sababu hospitali zipo mbali sana eneo hilo na ili kupata huduma yakupasa kutembea umbali wa kilometa 1000. Kuna madaktari wachache na hakuna wataalam wa upasuaji.
Ikiwa makazi yana watu wapatao 100 ambao wengi wao ni wanasayansi na wafanyakazi wa Jeshi la Anga na Maji la Chile, wale wenye kufanya kazi na jeshi huleta familia zao.
Hii inamaanisha kuna ofisi ya posta, shule ndogo, benki na vifaa vingine vya msingi. Je! Ni maisha ya namna gani wanaishi wakazi wa eneo hili? Bila shaka ni swali ambalo kila mtu atajiuliza.... Endelea kufuatilia blogu yako pendwa ya DundiikaNews ili kujua zaidi katika kijiji hiki.
Na Grace Mkanyago.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

KIFAHAMU KIJIJI CHA BARAFU AMBAPO ILI KUISHI INABIDI UTOLEWE KIDOLE TUMBO (APPENDIX)
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
9/08/2018 04:15:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: