Loading...

LUPITA MBIONI KUNYAKUA TUZO NYINGINE KUBWA YA FILAMU

Loading...
Muigizaji maarufu wa Hollywood wa nchini Kenya anatizamia kunyakua tuzo nyingine ya pili ya Oscar mwaka kesho.

Lupita alishinda tuzo yake ya kwanza ya Oscar kama Muigizaji Bora wa Kike Msaidizi wa mwaka 2013 kupitia uhusika alioucheza katika filamu ya kihistoria ya '12 Miaka ya Utumwa/12 Years a Slave'

Anatarajia kupokea tuzo ya pili katika msimu wa 91 wa tuzo za Oscar mwaka ujao na washirika wenzake katika filamu ya 'Black Panther' kwa kipengele cha Picha Bora ya Mwaka.

Waigizaji wenzake katika filamu ya 'Black Panther' ambao wamekusanya zaidi ya dola bilioni 1.3 kama mauzo ya duniani kote, wameanza kampeni kwa ajili ya filamu hiyo ili kushinda tuzo hiyo.

"Hatujui ni nini, kwahiyo sijui nifurahi kwa hili au la. Ninachoweza kusema ni kwamba. Kama kuna kampeni ya picha bora ya mwaka basi filamu yetu ndio inapaswa kuangaziwa," muigizaji mkuu Chadwick Boseman alinukuliwa na ripota wa Hollywood.

Tuzo hizo hazijawahi kuchagua na wala kutoa tuzo kwa filamu za superhero. Hata hivyo kufuatia mafanikio makubwa ya sinema ya 'Black Panther' 'A Star is Born' na 'Avengers: Infinity War' na umaarufu wa filamu hizo duniani kote hata kufanya kuchaguliwa katika vipengele vya filamu maarufu.
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
LUPITA MBIONI KUNYAKUA TUZO NYINGINE KUBWA YA FILAMU LUPITA MBIONI KUNYAKUA TUZO NYINGINE KUBWA YA FILAMU Reviewed by By News Reporter on 9/21/2018 10:41:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.