Loading...
Katika jukumu la kuhakikisha maisha ya wapenzi wa muziki yanaokolewa huko nchini Zimbabwe, matamasha makubwa mawili ya burudani yaliyotarajiwa kufanyika mjini Harare katika wiki kadhaa zijazo yameahirishwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Tamasha la RSVP lililopangwa kufanyika ukumbi wa Glamis Arena Jumamosi hii, ikijumisha wasanii wakubwa kama Cassper Nyovest na Prince KB wa Afrika Kusini, limerushwa hadi Novemba 10 huku Shoo ya Ammartia Ignite ambayo ingepambwa na wasanii kama Ammara Brown na Nyota kutoka Naija Mr Eazi imerushwa mbali zaidi.
Waandaaji wa tamasha la RSVP walisema wamefikia uamuzi huo baada ya kushauriana na Wizara ya Afya na Huduma ya Watoto, Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA), na Halmashauri ya Jiji la Harare moja ya wadau wengine.
"Tumeguswa na madhara ya kiafya kwa umma endapo tungeendelea na tamasha hilo kwa sababu tulilenga kuuza vyakula na vinywaji siku ya tukio.
"Tunaufahamu katika maswala ya afya na tunawajali watu kwahiyo tumeahirisha hadi Novemba. Tumewaomba radhi wasanii wetu Cassper Nyovest, Prince KB na wasanii wengine waliotakiwa kutumbuiza tamashani," alisema moja ya muandaaji wa tamasha Kush Zvirawa.
Japo kuna baadhi ya shoo na matamasha bado yanaendelea na ratiba zake kama kawaida. Hadi sasa ugonjwa huo wa kipindupindu ambao chanzo chake ni uchafu umekuwa tishio nchini humo na vifo vya watu kadhaa vimeripotiwa.
Na Mary Mkeu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

ZIMBABWE: UGONJWA WA KIPINDUPINDU TISHIO, MATAMASHA YAHAIRISHWA
Reviewed by By News Reporter
on
9/21/2018 11:38:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: