Loading...

WILIAN AIBEBA CHELSEA MASHINDANO YA EUROPA

Loading...
Chelsea ilianza mashindano ya Europa League kwa ushindi baada ya kushinda PAOK Thessaloniki FC 1-0 katika uwanja wa Toumba.

Nyota wa Brazil Willian aliifungia the Blues dakika ya saba baada ya mechi kuanza, baada ya kusaidiwa na Ross Barkley.

Mabingwa hao wa FA wameonekana kuendelea vizuri tangu kuanza kwa msimu, baada ya kushinda mechi zao tano za mwanzo EPL.

Maurizio Sarri aliwapa mapumziko wachezaji wake nyota akiwemo Eden Hazard na wengine wanne baada ya kuilaza Cardiff City katika mechi kati yao Stamford Bridge wikendi iliyopita.

Kocha Coach Razvan Lucescu alimleta uwanjani Amr Warda kuchukua mahali pa Dimitrios Pelkas katika dakika ya 62.

Pia Marcos Alonso alichukua mahali pa Cesar Azpilicueta katika dakika ya 65, hatua iliyoweka Chelsea kifua mbele katika mechi hiyo. 

PAOK Thessaloniki pia ilifanya mabadiliko mengine katika dakika ya 70 kwa kumleta Aleksandar Prijovic kuchukua mahali pa Yevhen Shakhov.

Dakika ya 80, Chelsea ilifanya mabadiliko pia kwa kumwondoa uwanjani Alvaro Morata na kumleta Olivier Giroud.

Chelsea haijashindwa tangu msimu wa Ligi ya Premier kuanza. Wikendi, ilishinda Cardiff 4-1 Stamford Bridge.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WILIAN AIBEBA CHELSEA MASHINDANO YA EUROPA WILIAN AIBEBA CHELSEA MASHINDANO YA EUROPA Reviewed by GEOFREY MASHEL on 9/21/2018 09:31:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.