Loading...

'MAJIVUNO NA KIBURI CHA PESA HAVITONIISHA', MAYWEATHER ADAI ALITESEKA SANA MPAKA KUFIKA HAPO

Loading...
Bondia bingwa wa uzani wa chini wa Marekani aliyestaafu Floyd Mayweather aliwashambulia watu wanaomchukia kutokana na kiburi alichonacho na kuwafunga midomo.

Bondia huyo aliyesifiwa kwa miaka kadhaa na kushinda tuzo za bondia bora mara sita (2007 – 2010, 2012 – 2014) alifunguka kwenye mtandao wa Instagram kwa nini ana kiburi na majivuno.

Maisha ya kifahari ya Mayweather kwanzia kusafiri kwa ndege yake ya kibinafsi na kuonyesha pesa nyingi alizo nazo yanaweza kumwacha shabiki wake na maswali mengi.

Hata hivyo, kutokana na umaarufu wake, mambo sio rahisi kwa Mayweather ambaye alisisitiza kuwa ana haki ya kuwa na kiburi kinachotokana na mali nyingi anazomiliki.

Bondia huyo alidai kuwa alikuwa na maisha ya umaskini kabla ya kujiweza na kuwa tajiri. 

“Kabla ya ndege, motaboti ya kisasa, Bugatti na mengine, Niikuwa na matatizo, Nilitoka kwenye umaskini hadi matawi ya juu. Wengine hunizungumzia kwa kuwa na kiburi, lakini nina haki ya kuwa hivyo, 

“Tunaishi katika dunia ambayo watu wanataka kuridhishwa mara moja. Nilifanya kazi kwa bidii maisha yangu yote, nitastaafu bila kushindwa na kuwekeza kwa viwango vikubwa, hivyo nina haki ya kuishi maisha mazuri zaidi,” posti ya Mayweather ilisema.

Mayweather amegonga vichwa vya habari kwa zaidi ya miaka 10 ya taaluma yake kama bondia, lakini matamshi yake kwenye vikao vya wanahabari vimezua maswali kuhusu tabia zake mara kwa mara.

Mara nyingi, aliwapuuzia mbali wapinzani wake, moja kati ya matukio kama hayo yaliyozungumziwa sana ikiwa dhidi ya Manny pacquiao ambapo alidaiwa kutumia lugha ya madharau kueleleza kuwa angemshinda raia huyo wa Ufilipino.
Na Catherine Kisese.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
'MAJIVUNO NA KIBURI CHA PESA HAVITONIISHA', MAYWEATHER ADAI ALITESEKA SANA MPAKA KUFIKA HAPO 'MAJIVUNO NA KIBURI CHA PESA HAVITONIISHA', MAYWEATHER ADAI ALITESEKA SANA MPAKA KUFIKA HAPO Reviewed by By News Reporter on 9/07/2018 01:20:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.