Loading...
Wakazi wa vijiji viwili katika kata ndogo ya Ainamoi kaunti ya Kericho - Kenya wamejawa na hofu baada ya watu wasiojulikana kukata sehemu za siri za ng'ombe wanajawazito.
Inasemekana watu hao pia wanang'oa jicho la ng'ombe na wanahakikisha amekufa kabla ya kuondoka.
Wafugaji wa ng'ombe katika vijiji hivyo wameonywa dhidi ya visa vya aina hiyo na sasa wengi wao wanataka serikali iingilie kati ili iwakamate washukiwa.
Chifu wa eneo hilo Stephen Sang alidhibitisha kisa hicho na kusema kuwa kilitokea katika kijiji cha Kirupta katikati mwa mwezi Agosti ambapo ng'ombe wa kwanza alikatwa sehemu zake za siri pamoja na jicho kung'olewa.
" Watu wanaotekeleza vitendo hivyo ni kama wanalenga ng'ombe ambao ni wajawazito tu. Kwa mara ya kwanza kisa hiki kilitokea majuma matatu yaliopita katika kijiji ha Krupta ambapo ng'ombe mmoja wa aina ya Ayshire ambaye alikuwa mjamzito alipatikana akiwa amefariki na sehemu zake za siri zilikuwa zimendolewa pamoja na jicho," Sang alisema.
John Tonui ambaye alikuwa mfugaji wa ng'ombe huyo, alisimulia jinsi amepata hasara na anahofia kwamba ng'ombe wake wengine huenda watauawa kupitia njia hiyo.
"Tulienda kulala jana saa nne usiku ila hatukusikia msukosuko wowote, la kushangaza niliamuka asubuhi na nikagundua kwamba ng'ombe wangu alikuwa amaekatwa sehemu za siri na jicho lake la mkono wa kulia nimeng'olewa," Tonui alisema.
Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: WATU WASIOJULIKANA WAIBUKIA KUSAKA NYETI ZA NG'OMBE
Reviewed by By News Reporter
on
9/07/2018 02:28:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: