Loading...
Maafisa wa afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametangaza kuwa sasa virusi vya maradhi ya Ebola vimedhibitiwa, ikiwa ni wiki tano tangu kuripotiwa mripuko mpya wa maradhi hayo uliopelekea watu 89 kufariki dunia mashariki mwa nchi hiyo.
Mnamo Agosti Mosi, wizara ya afya ya Kongo ilitangaza mripuko wa maradhi hayo katika jimbo la Kivu Kaskazini na Alhamisi iliyopita ikasema virusi vya ugonjwa huo vimesambaa hadi katika mji wa Butembo wenye wakaazi wapatao milioni moja.
Waziri wa Afya, Dk. Oly Ilunga Kalenga, amesema tangu tarehe 13 Agosti hakujawa na wagonjwa wapya wa Ebola, hali inayoashiria kuwa mripuko huo umedhibitiwa katika maeneo ya mji wa Mabalako.
Taarifa kuhusiana na hofu kuwa huenda maradhi hayo yakasambaa zaidi zilianza kusikika Alhamisi baada ya watu wawili kuripotiwa kufariki dunia katika mji wa kibiashara wa Butembo unaopakana na nchi jirani ya Uganda.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259

UGONJWA WA EBOLA WADHIBITIWA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO
Reviewed by By News Reporter
on
9/09/2018 12:06:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: