Loading...

AFISA MAARUFU WA POLISI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI UGANDA

Loading...
Watu waliokuwa na bunduki wamemuua afisa mmoja maarufu wa polisi nchini Uganda pamoja na mkewe.

Msemaji wa jeshi la polisi, Emilian Kayima, amesema afisa huyo, Muhammad Kirumira, alishambuliwa wakati alipokuwa akiendesha gari jirani na makazi yake yaliyoko nje ya mji mkuu, Kampala. 

Kirumira aliibuka kuwa maarufu mapema mwaka huu baada ya kujiuzulu wadhifa wa ukamanda wa wilaya kufuatia mzozo kati yake na maafisa wa ngazi za juu aliowatuhumu kwa rushwa na uhalifu mwingine. 

Alitiwa mbaroni na kufikishwa mahakama ya jeshi la polisi iliyompata na hatia ya kutumia vibaya mamlaka yake na ikapendekeza ashushwe cheo. Hata hivyo, Kirumira alikanusha mashitaka dhidi yake. 

Waganda wengi wameandika ujumbe katika ukurasa wa Twita wakilaani kuuawa kwa afisa huyo wa polisi. 

Mivutano ya kisiasa imekuwa ikiongezeka nchini Uganda kufuatia kukamatwa hivi karibuni kwa mwanamuziki na mbunge wa upinzani Bobi Wine anayemkosoa Rais Yoweri Museveni.
Na Hamisi Fakhi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
AFISA MAARUFU WA POLISI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI UGANDA AFISA MAARUFU WA POLISI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI UGANDA Reviewed by By News Reporter on 9/09/2018 11:54:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.