Loading...

WAVAMIZI WA MISITU KUKIONA CHA MTEMAKUNI

Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde amesema ni wakati muafaka kwa Serikali kuangalia uwezekano wa kurekebisha sheria za misitu na kuzifanya ziwe kali zaidi.

Alisema hilo litasaidia kupunguza uharibifu wa hifadhi za misitu nchini unaofanywa kwa makusudi na watu wanaovamia misitu.

Malunde alisema hayo alipotembelea Msitu wa Nyantakara akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalam ya wilaya na maofisa wa Wakala wa Misitu (TFS) kwa lengo la kuona uvamizi na uharibifu unaondelea katika hifadhi za misitu iliyopo wilayani humo.

Katika ziara hiyo Malunde alikuta msitu huo ukiwa umevamiwa na kuharibiwa kwa kiasi kikubwa.

Kutokana na hali hiyo, aliagiza wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya hifadhi ya Biharamulo na Nyantakara kuondoka kabla ya kuwachukulia hatua za kisheria.

"Msitu huu (Nyantakara) unavamiwa kwa
Loading...
kasi kubwa na kuharibiwa na watu wanaondesha shughuli za kilimo na ufugaji kinyume cha sheria,

"Hali hii inatisha zaidi baada ya Serikali kupandisha hadhi mapori tengefu ya Kimisi, Burigi na Biharamulo kuwa Hifadhi za Taifa ambapo kuna sheria kali zinazowabana wananchi kufanya shughuli za kibinadamu.

"Nikiwa kiongozi mwenye dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria. Sitakubali hali hii iendelee, nawataka muondoke kwa hiari na kwenda kusihi kwenye vijiji vinavyotambulika kisheria kabla Serikali haijatumia nguvu kuwaondoa," alisema.

Mtendaji mkuu wa TFS, Professa Dos Santos Silayo alisema kwamba vijiji ambavyo vinaanzishwa katika maeneo ya misitu bila kufuata taratibu ni kosa kisheria na kuahidi kushirikiana kudhibiti uvamizi na uharibifu wa misitu wilayani hapa.

Meneja Misitu wa Kanda ya Ziwa, Cosmas Ndakidemi aliwataka wakazi wanaoishi maeneo ya jirani na misitu ya hifadhi ya Biharamulo na Nyantakara kuheshimu mipaka na taratibu zilizopo ili kuepuka kuingia kwenye mkono wa sheria.
Na Shaibu Ramadhani.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
WAVAMIZI WA MISITU KUKIONA CHA MTEMAKUNI WAVAMIZI WA MISITU KUKIONA CHA MTEMAKUNI Reviewed by By News Reporter on 9/27/2018 07:29:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.