Loading...

ZANZIBAR: OMAN YAONGEZA NGUVU UKARABATI MAJUMBA YA KALE, KUONGEZA CHACHU KWA WATALII

UJUMBE wa Idara ya Nyaraka na Kumbukumbu ya za Kale kutoka Oman, umesema utaendelea kuisaidia Zanzibar katika ukarabati wa majengo ya kihistoria ili iwe chachu ya kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Uhifadhi Nyaraka na Kumbukumbu ya Oman Dk. Hamed Mohammed Al Dhawiyan, amesema hayo jana wakati ujumbe huo ulipofanya ziara maalumu kuangalia magofu ya Maruhubi, Kijichi, na Kasri ya Mtoni ambayo zamani yalikuwa makaazi ya wafalme mbalimbali.

Alisema kuyaimarisha majengo hayo yenye historia ya kuvutia na kuyarejeshea hadhi yake, kutayaweka katika hadhi yake ya zamani na kuwa kivutio kikubwa kwa watalii na wageni wengine wanaofika Zanzibar.

Loading...
ily: Verdana, sans-serif;">Alisema maeneo hayo ya kumbukumbu za kihistoria ni muhimu kwa maslahi ya Zanzibar, na kwamba iko haja ya kuyatunza vyema na kuyatumia kiuchumi ili kuongeza pato la taifa.

“Ni vizuri majengo haya yawekwe katika mpango wa kufanyiwa matengenezo ili yawe imara na kudumu kwa muda mrefu. Tukifanya hivyo hata Waomani watapata hamu ya kuyatembelea kila wafikapo hapa,” alisema.

Aidha alisema ni jambo la kijivunia kwamba Oman na Zanzibar ambazo zina udugu wa damu na wa kihistoria, zinakaa pamoja na kupanga mikakati ya kusaidiana katika sekta mbalimbali za kiuchumi, kijamii na utamaduni.

Naye Mkuu wa kitengo cha Makumbusho na Mambo ya Kale, Abdalla Khamis Ali, alisema ujio wa ujumbe huo nchini utaleta matunda na neema kwa Zanzibar hasa katika kuyahuisha majengo hayo.
NA Mohamedi Makame.




Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
ZANZIBAR: OMAN YAONGEZA NGUVU UKARABATI MAJUMBA YA KALE, KUONGEZA CHACHU KWA WATALII ZANZIBAR: OMAN YAONGEZA NGUVU UKARABATI MAJUMBA YA KALE, KUONGEZA CHACHU KWA WATALII Reviewed by GEOFREY MASHEL on 9/06/2018 11:16:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.