Loading...
Watu 50 wamefariki dunia nchini Kenya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali kwenye barabara kuu ya Nairobi-Kisumu.
Walioshuhudia wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea leo mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.
Ajali hiyo mbaya ilitokea katika eneo la Fort Ternan Kaunti ya Kericho.
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ni miongoni mwa waliotuma salamu za rambirambi kwa Wakenya.
Ameandika: "Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya basi iliyotokea Kericho nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50. Nakupa pole Mhe. Rais Uhuru Kenyatta, familia za marehemu na Wakenya wote. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema na majeruhi wapone haraka."
"Mungu azilaze roho za marehemu ndugu zetu mahali pema peponi, AMINA."
Na Hamisi Fakhi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

AJALI YA BASI YAUA 50 KENYA, MAGUFULI ATUMA RAMBI RAMBI
Reviewed by By News Reporter
on
10/10/2018 06:01:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: