Loading...
Mwanamke mmoja nchini Uganda ameshangaza wengi baada ya kujioa mwenyewe.
Lulu Jemimah mwenye umri wa miaka 32 alijioa mwezi Agosti jijini Kampala na kudai kuwa kwa miaka kadhaa watu wamekuwa wakimuuliza kuwa lini angefunga ndoa.
"Nikiwa na miaka 16 baba yangu aliandika hotuba yake kwa ajili ya kuisoma siku ya harusi yangu. Kila nilipokuwa nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa mama yangu alikuwa akiniombea, na kwa miaka ya karibuni maombi yake yalikuwa pamoja na kupata mume bora, ambaye atanifaa," amesema Bi Jemimah.
Mwaka jana Bi. Jemimah alichaguliwa kujiunga na masomo ya juu ya uandishi wa ubunifu katika chuo kikuu maarufu cha Oxford nchini Uingereza. Lakini licha ya mafanikio hayo ya kielemu anasema bado watu waliendelea kumuuliza anapanga kuolewa lini, ili aanzishe familia na kupata watoto.
Kutokana na hali hiyo, Jemimah anasema aliamua kuchukua uamuzi wa kuwatuliza; "Nilipotimiza miaka 32 nikaamua kujioa. Naamini mimi nitajitunza na kujipa amani." Na alidai gharama ya harusi yake iligharimu dola $2.62 sawa na Sh 5700 pesa za Tanzania na pesa hiyo ilitumika kama gharama ya nauli kumpereka mahali pakufungia ndoa ila kila kitu aliazima kwa rafiki zake.
Na Gabriel Paschal.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

LULU JEMIMAH MWANAMKE 'ALIYEJIOA' MWENYEWE
Reviewed by By News Reporter
on
10/10/2018 06:29:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: