Loading...

BASHIRU ASEMA CCM BADO KUNA MIJIZI

Loading...
KATIBU Mkuu wa (CCM), Dk. Ally Bashiru, amesema amekuta wizi wa kutisha ndani ya chama hicho uliofanywa na watu wenye majina makubwa na kwamba iwapo ataamua kutaja majina yao, umma utashangaa na kushindwa kuamini.

Sambamba na wizi, amesema hali katika chama hicho si njema kwa sababu amekuta matatizo matatu makubwa ambayo ni itikadi, nidhamu na utegemezi.

"Tangu nimeingia kwenye chama changu nimekuta matatizo matatu. La kwanza ni tatizo la kutokuwa na mtazamo wa pamoja nini mnatakiwa kufanya. Mnabishana nyie kwa nyie. Kwa hiyo suala la kiitikadi ambalo litawapa mtazamo wa pamoja ni tatizo kubwa zaidi ndani ya CCM kuliko vyama vingine," alisema.

Alisema CCM bado inasimamia misingi ya Azimio la Arusha, hivyo asiyetaka kusimamia misingi hiyo aondoke kwa kuwa kukiwa na mtazamo wa pamoja wa kiitikadi, watasimamia haki ya walio wengi.

Dk. Bashiru aliyasema hayo jana wakati akijibu maswali katika mdahalo wa Kumbukumbu ya Miaka 19 ya Mwalimu Julius Nyerere, uliopewa jina la 'Mienendo ya Uchaguzi na Mustakabali wa Mataifa ya Afrika', uliofanyika katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Na Ally Hussein.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
BASHIRU ASEMA CCM BADO KUNA MIJIZI BASHIRU ASEMA CCM BADO KUNA MIJIZI Reviewed by By News Reporter on 10/13/2018 08:22:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.