Loading...
LEO ikiwa ni siku ya tatu tangu kutekwa kwa mfanyabishara maarufu nchini, Mohamed Dewji, maarufu kama Mo Dewji. Jeshi la Polisi limeendelea na msako mkali katika maeneo mbalimbali ya mipaka, viwanja vya ndege na maeneo ya baharini.
MO alitekwa juzi alfajiri na watu wanaodaiwa kuwa raia wa kigeni katika hoteli ya Colloseum alikokuwa akifanya mazoezi ya viungo.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, aliviambia vyombo vya habari kuwa wanaendelea na msako kumtafuta mfanyabiashara huyo.
"Tunaendelea na uchunguzi lakini mpaka sasa hatuna habari mpya. Tumeweka doria na msako katika maeneo mbalimbali kama viwanja vya ndege, bandarini na kwenye mipaka," alisema Mambosasa.
Pia alisema bado wanaendelea kuwashikilia watu 12 waliokamatwa juzi wakiwamo walinzi wa hoteli, walinzi wa nyumbani kwa Mo, walinzi wa kazini kwake na baadhi ya wafanyakazi wake.
Mambosasa alisema bado wanaendelea kuwahoji wale wanaowashikilia ikiwa jitihada za kupata taarifa zitakazowezesha kumpata Mo na wahusika waliofanya uhalifu huo.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

ULINZI KILA KONA MSAKO WA MO DEWJI
Reviewed by By News Reporter
on
10/13/2018 08:31:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: