Loading...

SHILOLE AWATAKA VIJANA KUJIONGEZA

Loading...
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Shilole, amewataka wasanii wenzake, vijana na akina mama kuchangamkia fursa ya huduma ya SimAkaunti ya Benki ya CRDB ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.

Akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya wiki kuwapata washindi, Shilole, ambaye pia ni balozi wa huduma hiyo, alisema kwa kutumia huduma ya SimAkaunti vijana wanaweza wakabadili maisha yao kwa kunufaika na zawadi watakazozipata.

"Mimi ni mmoja wa watu ninayetumia huduma hii, wasanii wenzangu, vijana, akina mama tuchangamkie fursa hizi," alisema Shilole.

Aliongeza kuwa huduma hiyo ya CRDB inarahisisha mambo na mtu hapaswi kutembea na kiasi kikubwa cha fedha  mkononi kwa sababu inatoa fursa kwa watu kufanya malipo na manunuzi bila usumbufu.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Benki hiyo, Ariel Mkony, aliwataja washindi wa wiki hiyo kuwa ni Cuthbert Mwantambula mkazi wa Mkoa wa Lindi ambaye alijishindia Sh. milioni mbili na Adela Mohammed wa Tanga ambaye yeye alijishindia Sh. milioni moja.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SHILOLE AWATAKA VIJANA KUJIONGEZA SHILOLE AWATAKA VIJANA KUJIONGEZA Reviewed by By News Reporter on 10/13/2018 08:47:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.