Loading...

LOWASSA: WANANCHI WAMEJAZWA HOFU

Loading...
MJUMBE wa Kamati Kuu ya (Chadema) na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amesema wananchi wamejazwa hofu inayowafanya wachague watu ambao hawakuwapenda wakati wa uchaguzi.

Lowassa aliyasema hayo jana wakati wa mdahalo wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mdahalo huo wa kumbukizi ya miaka 19 ya Tanzania bila Mwalimu Julius Nyerere, ulipewa jila la 'Mienendo ya Uchaguzi na Mustakabali wa Mataifa ya Afrika' na kuhudhuriwa na wanasiasa, wasomi na wadau wengine.

Alitoa mfano kuwa  binafsi alishangaa kuona Landrover 45 za polisi zikiranda randa kwenye Jimbo la Monduli wakati wa uchaguzi mdogo jambo ambalo alisema liliwatia hofu wananchi.

"Mimi naona nchini kuna tatizo la hofu na chuki. Inajengwa  hofu kubwa sana kwa wananchi wakati wa uchaguzi. Pale Monduli tulifanya uchaguzi, kale kamji ni kadogo sana lakini kulikuwa na Landrover 45 za polisi na magari manne ya upupu, utafikiri kuna vita na hivi vinafanywa kutumia vyombo vya dola kusimamia uchaguzi," alisema.

Lowassa alisema ni muda mwafaka nchi ikatazama utaratibu viongozi watazungumza na wananchi ili kuondoa chuki na hofu na mambo yaliyoandikwa kwenye Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba yachukuliwe.
Na Salim Juma.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
LOWASSA: WANANCHI WAMEJAZWA HOFU LOWASSA: WANANCHI WAMEJAZWA HOFU Reviewed by By News Reporter on 10/13/2018 08:52:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.