Loading...
MKUU wa Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Rachael Kasanda, amewataka wanawake mkoani humo kutokubali kufanya tendo la ndoa na wanaume ambao hawajafanyiwa tohara, maarufu kama 'mkono wa sweta', ili kuepukana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU).
Kasanda alitoa ushauri huo jana wakati akizinduzia kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha wananchi, hususan wanaume, kupima VVU na kuanza kutumia dawa za kufubaza virusi vya ugonjwa huo (ARV).
Alisema hayo katika hafla hiyo iliyofanyika kimkoa katika kata ya Majimoto, Halmashauri ya Mpimbwe, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makala.
Alisema kuwa wanawake ambao wamekuwa wakifanya tendo la ndoa na wanaume ambao hawajafanyiwa tohara wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa.
Alisema kuwa anawashauri wanawake wa mkoa huo kutokubali kufanya tendo la ndoa na mwanaume yeyote ambae atakuwa hajafanyiwa tohara.
“Hata kama mwanamume atataka kutoa pesa nyingi kiasi gani, msikubali mpaka awe amefanyiwa tohara ndipo uweze kufanya naye tendo hilo,” alisema.
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wanaume wenye umri mkubwa kutoona aibu kufanyiwa tohara kwa kuwa hata wakifanyiwa hakuna mtu ambaye atajua.
Na Haika Gabriel.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

DC KATAVI: MSIWAKUBALI WANAUME WENYE 'MKONO WA SWETA'
Reviewed by By News Reporter
on
10/11/2018 07:51:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: