Loading...

HERI YA SIKU YA KUZALIWA RAIS DKT. MAGUFULI

Loading...
Tunapenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kote nchini kumtakia heri ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.

Ni Oktoba 29, 1959 ni siku ambayo Mwenyezi Mungu alitupa Watanzania zawadi ya Mtoto John Pombe Magufuli ambaye Leo hii amekuwa lulu, Mkombozi, Shujaa, Mtetezi, Mlezi, Mjenzi wa Watanzania. Leo hii ni nembo ya uongozi wa mfano Afrika na Duniani kote.

Dkt. Magufuli ametumia nguvu na akili zake zote kuhakikisha mitandao ya Barabara, Madaraja yanajengwa nchi nzima  na Leo anajenga Reli ya kisasa ya umeme kwa kiwango cha standard gauge pasipo kusahau kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania kwa kununua ndege mpya saba.

Kwa kupitia uzalendo na uchapakazi wake Leo hii elimu inatolewa bure nchi nzima; rushwa na ufisadi anavipiga vita kwa vitendo; rasilimali za Taifa anahakikisha zinalindwa vilivyo ili kumnufaisha Mtanzania n.k.

Kwa ufupi maisha yake yamekuwa ya msaada mkubwa kwa Watanzania kwani ameonyesha uwezo mkubwa wa kupambana na Maadui zetu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini. 

Pia ameonyesha mapenzi ya dhati ya kusimama  upande wao Watanzania Wanyonge yaani Wakulima, Wafanyakazi, Wavuvi na Wafugaji kote nchini. Watanzania wanyonge hawana la kukulipa zaidi ya kukutakia Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu yenye baraka tele, uendelee kuwatumika vyema Watanzania.

Heri ya Kuzaliwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Na Hamisi Chambo.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
HERI YA SIKU YA KUZALIWA RAIS DKT. MAGUFULI HERI YA SIKU YA KUZALIWA RAIS DKT. MAGUFULI Reviewed by By News Reporter on 10/29/2018 07:48:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.