Loading...

MAUAJI YA KHASHOGGI, SAUDIA ARABIA WAKALIWA KOONI

Loading...
Saudi Arabia imekubali kuwa Mwandishi wa habari Jamal Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi wa Saudia nchini Turkey baada ya mapigano kutokea.

Habari hiyo imetangazwa na television ya taifa hilo, ambayo imesema kuwa mapigano hayo yalikuwa kati ya Khashoggi na watu aliokutana nao ndani ya ubalozi huo ambayo yalisababisha kifo chake.

Watu 18 wamekamatwa mpaka sasa kuhusiana na kifo hicho cha mwandishi huyo.

Khashoggi alipotea Oktoba 2 baada ya kwenda ubalozi wa Saudi Arabia huko Instanbul ili kupata nyaraka za kumuoa mchumba wake wa Kituruki, Hatice Cengiz.
Na Ramadhani Sharia.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAUAJI YA KHASHOGGI, SAUDIA ARABIA WAKALIWA KOONI MAUAJI YA KHASHOGGI, SAUDIA ARABIA WAKALIWA KOONI Reviewed by By News Reporter on 10/20/2018 11:39:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.