Loading...

MIILI 17 YAPATIKANA MAPOROMOKO YA MATOPE UGANDA

Loading...
Idadi isiyo julikana ya watu wamepoteza maisha kufuatia maporomoko ya matope katika wilaya ya Bududa mashariki mwa Uganda karibu na mlima Elgon, katika kile maafisa wanataja kuwa ni maporomoko makubwa na hatari kuwahi kushuhudiwa.

Kwa mujibu wa wakazi wa wilaya ya Bududa, kata ndogo ya Bukalasi, yenye milima mingi, maporomoko ya matope yalianza kushuhudiwa saa nane alasiri, wakati maji, matope, na miti ikiporomoka kutoka juu ya mlima, kufunika makao ya watu hadi sehemu tambarare madukani.

Maafisa wa uokoaji walichelewa eneo la tukio wakati tukio limetokea lakini wakazi wa eneo hilo wenye ujasiri wakijitwika jukumu la kuwaokoa wenzao.

“Nyumba zimefunikwa na udongo. Kituo cha kibishara nacho kimefunikwa kiasi kwamba huwezi kujua kama kilikuwepo. Kwa sasa tunaogopa kuwaokoa wenzetu kwa sababu huwezi kujua, maporomoko makubwa Zaidi yanaweza kutokea tena,” ameongezewa Wakikona.

Zaidi ya watu 100 walikufa baada ya kutokea maporopoko ya ardhi katika wilaya hiyo ya Bududa mwaka 2010.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MIILI 17 YAPATIKANA MAPOROMOKO YA MATOPE UGANDA MIILI 17 YAPATIKANA MAPOROMOKO YA MATOPE UGANDA Reviewed by By News Reporter on 10/12/2018 07:38:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.