Loading...

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO AJINYONGA HADI KUFA

Mwanafunzi mmoja wa shule ya secondary ya Sengerema high school aitwaye Ayoub Yahya Petro , miaka 19, anayesoma kidato cha 5 mchepuo wa PCB, mwenyeji wa Kyerwa-Kagera, amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya neti (chandarua) aliokua ameifunga kwenye mti uliopo pembeni ya uwanja wa mpira wa shule hiyo, iliyopo Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Tukio hilo limetokea jana tarehe 18.10.2018 majira ya saa 06:00 asubuhi, hii ni baada ya wanafunzi wenzake kupita eneo la uwanja wa shule kisha kuona mwili wa marehemu ukiwa unaning’inia juu ya mti na kutoa taarifa kwenye uongozi wa shule ambao ulifikisha taarifa hizo kituo cha polisi.

Polisi tulifanya ufu
Loading...
tiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu mahali hapo. Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafaamika, Polisi bado tunaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya DDH Sengerema kwa ajili ya uchunguzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya mazishi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linatoa wito kwa wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Na Joshua Filemoni.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO AJINYONGA HADI KUFA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO AJINYONGA HADI KUFA Reviewed by By News Reporter on 10/19/2018 06:04:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.