Loading...

PASTA AKAMATWA AKIENDESHA IBADA HUKU WAUMINI WAKIWA UTUPU

Loading...
Pasta mmoja na waumini wake saba wa kike walikamatwa nchini Uganda kwenye nyumba moja walipokuwa wakiendesha ibada wakiwa uchi kama walivyozaliwa.

Wanawake hao wanasemekana kuendesha maombi hayo wakiwa bila hata chupi mbele ya pasta wao siku ya Jumanne, Oktoba 2.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mirror, nane hao ambao ni wa kanisa la Full Gospel walipatikana na maafisa wa polisi kwenye nyumba moja eneo la Rukiga. 

Kulingana na mkuu wa wilaya hiyo Emmy Ngabirano, ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kuwa wanawake hao wote walikuwa katika ndoa.

Ngabirano alishtumu kitendo hicho huku akidokeza kuwa kanisa walilodai kuwa wanachama wake halijasajiliwa kwa mujibu wa sheria. 

"Tunaheshimu uhuru wa kuabudu lakini watu wanatakiwa kufuata sheria zilizopo za kuendesha kanisa na mojawapo ya sheria hizo ni liwe limesajiliwa. Waliokamatwa wanaendesha mikutano haramu nyumbani kwa mtu ambapo wanadai kuwa kanisa walipopatikana wakiwa uchi," Alisema Ngabarino.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotufikia, wanawake hao hawakuwa tu wakifanya maombi wakiwa uchi bali pia hawakuwa makwao kwa wiki kadha.
Na Neema Bushubo.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
PASTA AKAMATWA AKIENDESHA IBADA HUKU WAUMINI WAKIWA UTUPU PASTA AKAMATWA AKIENDESHA IBADA HUKU WAUMINI WAKIWA UTUPU Reviewed by By News Reporter on 10/07/2018 07:19:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.