Loading...

ROONEY AWAPA MAKAVU MAN UTD

Loading...
Kapteni wa zamani wa Manchester United, Wayne Roon­ey amesema kuwa tatizo la timu hiyo siyo kocha Jose Mourinho bali wachezaji.

Rooney al­iondoka United akaenda Everton na msimu huu anaitumikia DC United ya Ligi Kuu ya Marekani, MLS.

Rooney ambaye ana aminika kuwa ni mchezaji makini sana, amese­ma kuwa wachezaji wa timu hiyo wanatakiwa kujitazama upya na kuanza kuipambania timu hiyo na siyo kuacha lawama zote kwa kocha Jose Mourinho.

Rooney amesema kama wachezaji hao wataonyesha ki­wango chao basi United inaweza kupata matokeo mazuri uwanjani.

Manchester Unit­ed wamekuwa na matokeo mabaya kwa siku za hivi karibuni na sasa wapo katika nafa­si ya nane wakiwa na pointi 13 tu wakiwa wame­sh­ache­za mich­ezo nane.

Wikiendi iliyopita timu hiyo ilipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle United, uki­wa ni wa kwanza kwao kuanzia Septemba 19.
Na Khalid Juma.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com
ROONEY AWAPA MAKAVU MAN UTD ROONEY AWAPA MAKAVU MAN UTD Reviewed by By News Reporter on 10/11/2018 06:52:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.