Loading...
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imepokea kibali Kumb. Na. FA.170/374/01/71 cha tarehe 24 Septemba, 2018 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni anawatangazia Wananchi wote raia wa Tanzania wenye sifa kuomba nafasi zilizoorodheshwa hapo chini:-
1. DEREVA DARAJA LA II - (NAFASI 8)
(a) Sifa za mwombaji:-
Kuajiriwa mwombaji awe mwenye cheti cha kidato cha nne (Form IV) na leseni
ya Daraja la E au C1 ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda
usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo
ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo
cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali. Waombaji wenye cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa
kwanza.
(b) Majukumu ya kazi:
(i) Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
(ii) Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
(iii) Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
(iv) Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
(v) Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari
(vi) Kufanya usafi wa gari, na
(vii) Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
Ngazi ya mshahara ni TGS B
MASHARTI KWA UJUMLA:
1. Mwombaji lazima awe raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu
yoyote ya Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
2. Mwombaji awe na Umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45 na awe
hajawahi kupatikana na kosa lolote la jinai, kufungwa jela na kufukuzwa kazi
katika Utumishi wa Umma.
3. Mwombaji aambatishe maelezo yake binafsi (CV)
4. Maombi yote yaambatane na nakala ya Vyeti vya uendeshaji magari (Taaluma),
vyeti vya kidato cha nne IV, cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi za hivi
karibuni na ziandikwe majina nyuma.
5. *Testimonials, provisional results, Statement of Results hati ya matokeo ya
kidato cha nne (FORM IV) RESULT SLIPS HAVITAKUBALIWA.
6. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika na NACTE na taarifa ya uhakiki iambatishwe
kwenye maombi
7. Uwasilishwaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria
8. Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono
9. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 24.10.2018 saa 9.30 alasiri.
Maombi yatumwe kwa Anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Manispaa Kigamboni,
S.L.P. 36009,
KIGAMBONI, DAR ES SALAAM.
Imetolewa na:-
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA KIGAMBONI.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA
Reviewed by By News Reporter
on
10/11/2018 06:55:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: