Loading...

WAZIRI WA FEDHA AJIUZULU AFRIKA KUSINI

Loading...
Waziri wa fedha wa Afrika Kusini Nhlanhla Nene amejiuzulu wadhifa wake baada ya kukubali kuwa aliwahi kukutana na familia ya Gupta ambayo inakabiliwa na mashtaka ya rushwa.

Rais Cyril Ramaphosa amesema amekubali uamuzi wa waziri huyo ili kulinda maslahi ya serikali.

Familia ya Gupta ambayo ni ya wafanyabiashara imekuwa ikituhumiwa kuwa na ukaribu usio wa kawaida na rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma ambapo yadaiwa walishirikiana katika kughushi mikataba ya serikal. Akina Gupta pia yadaiwa walikuwa na ushawishi katika uteuzi wa baraza la mazwaziri.

Ushawishi huo wa kina Gupta ulitafsiriwa kama 'kutekwa nyara' kwa serikali ya Zuma. Ingawa Gupta pamoja na Zuma wamekana madai hayo, lakini yalichangia pakubwa katika msukumo uliopeleka kung'oka madarakani kwa Zuma.

Nafasi ya Nene imechukuliwa na gavana wa zamani wa benki kuu ya nchi hiyo Tito Mboweni.

Hii ni mara ya tano tangu mwka 2014 kwa Afrika Kusini kubadili Waziri wa Fedha.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com
WAZIRI WA FEDHA AJIUZULU AFRIKA KUSINI WAZIRI WA FEDHA AJIUZULU AFRIKA KUSINI Reviewed by By News Reporter on 10/11/2018 07:22:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.