Loading...
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marufuku uuzaji wa tairi zilizotumika maarufu vipara kwamba haziruhusiwi tena kutumika.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Ngenya Athuman Yusuf leo Jumatano Oktoba 24,2018 imeeleza kuwa kuuza na kutumia tairi kipara ni kinyume na matakwa ya sheria namba 2 ya mwaka 2009.
“Tunawakumbusha wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa tairi za magari, pikipiki na baiskeli ambazo zilishatumika kwamba haziruhusiwi tena kutumika.”
“Tutaenda sambamba na ukaguzi utakaofanyika kwenye soko ili kubaini watakaokiuka agizo hili kwa kuendelea kufanya biashara ya kuuza au kusambaza tairi hizo,” amesema Dk Ngenya.
Katika taarifa hiyo amesema waagizaji na watumiaji wa tairi za magari kuwa umri wa tairi za magari ni miaka nane kutoka tarehe ambayo ilitengenezwa ambayo imeainishwa katika kila tairi.
“Tairi halitafaa kutumika baada ya umri huo bila kujali halijawahi kutumika kabisa, matakwa yanayotakiwa katika tairi za magari ikiwemo suala la umri yanapatikana kwenye kiwango cha Tanzania “TZS 617:2009 na TZS “618:2009,” Amesema Dk Ngenya.
Na Hamisi Shabani.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU BIASHARA YA MATAIRI YALIYOTUMIKA (USED)
Reviewed by By News Reporter
on
10/24/2018 05:39:00 PM
Rating:

Hindi ya upgrade truck rims 15' legends 16,
JibuFuta