Loading...

TAARIFA KWA UMMA: STARTIMES YAZITOA ITV, EATV NA STAR TV KATIKA VING'AMUZI VYAKE

Loading...

  • Star Media yafikia uamuzi wa kuondoa chaneli za ITV, STAR TV na EATV kutokana na sababu ya kutokuwa na Mikataba (SLA) au makabaliano.


  • Wamechukua kutoa taarifa kwa wateja wao na umma kwa ujumla kwamba, kutokana na sababu tajwa watasitisha matangazo ya chaneli tajwa hadi pale watakapo kuwa na makubaliano rasmi kwa mujibu wa sheria.


Kampuni ya Star Media (T) Limited (MUX) ambayo ina jukumu la kisheria la kurusha matangazo ya televisheni zenye leseni ya kurusha matangazo bure Nchini, chini ya Sheria, na vile vile Chaneli hizo zenye leseni za kurusha maudhui yao (CSP0 zina wajibu KISHERIA wa kusaini mikataba ya kurushwa na MUX yaani (SLA) ili kuweza kurushwa katika ving’amuzi vyao katika mfumo wa (FTA au wa kulipia kutokana na aina ya leseni) yaani ili watumiaji waweze kupokea matangazo yao kupitia ving’amuzi.

Kutokana na hilo, StarTimes imekua ikifanya juhudi mbali mbali kuhakikisha kwamba inaingia mikataba na chaneli hizo ili ziweze kurushwa kwa mujbu wa sheria, la sivyo inakua kinyume cha sheria kurusha chaneli bila kuwa na makubaliano (SLA) na chaneli iliyoko kwenye king’amuzi.

“HIVYO BASI, ni kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukirusha baadhi ya chaneli bila kuwa na makubaliano hayo hivyo tumefanya juhudi za makusudi kuhakikisha tunakubaliana na kuingia mikataba na chaneli hizo kwa mujibu wa Sheria za Nchi. 

Kwa juhudi hizo kwa ushirikiano na mamlaka husika, tumefanikiwa kuingia mikataba na baadhi chaneli Chaneli ila kwa baadhi ya chaneli imeonakena kuwa ngumu hata baada ya Mamlaka husika kuingilia kati, sababu kuu ikiwa ni maslahi ya kibiashara.

Hivyo basi kutokana na kushindikana kufikia muafaka wa makubaliano hayo, Star Media tumefikia uamuzi wa kuondoa chaneli za ITV, STAR TV na EATV kutokana na sababu ya kutokuwa na Mikataba (SLA) kwakuwa ni kinyume na Sheria kubeba chaneli hizo bila kuwa na mikataba au makubaliano.” Bw Wang Xiaobo, CEO StarTimes.

“HIVYO BASI tunapenda kutoa taarifa kwa wateja wetu na umma kwa ujumla kwamba, kutokana na sababu tajwa tutasitisha matangazo ya chaneli tajwa hadi pale tutakapo kuwa na makubaliano rasmi kwa mujibu wa sheria. Hivyo basi chaneli hizo zitaondolewa mara moja kutoka kwenye ving’amuzi vyetu.” Aliongeza Bw Wang.
Na Frank Malogo.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TAARIFA KWA UMMA: STARTIMES YAZITOA ITV, EATV NA STAR TV KATIKA VING'AMUZI VYAKE TAARIFA KWA UMMA: STARTIMES YAZITOA ITV, EATV NA STAR TV KATIKA VING'AMUZI VYAKE Reviewed by By News Reporter on 10/27/2018 11:26:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.