Loading...

VISA NA MIKASA: MWANAMKE MJA MZITO MBARONI KWA KUJARIBU KUNYOFOA ULIMI WA MUMEWE

Mwanaume mmoja nchini India yupo hoi taabani na hata kushindwa kuzungumza baada ya mkewe mwenye mimba ya miezi nane kumg'ata ulimi wake wakati akijaribu kumbusu wakati wa malumbano.

Kama unawaza busu la Kifaransa ndio njia nzuri zaidi inayovutia kutuliza ghadhabu za mwanamke wakati wa ugomvi na malumbano, basi kisa hiki kitakufanya ufikiri mara mbili pindi utakapo hitaji kutumia mbinu hiyo ili kumaliza malumbano.
Loading...
le="font-family: Verdana, sans-serif;">
Mwanaume, 22, kutoka Delhi, India, ilibidi akimbizwe hospitalini kwa matibabu baada kuonekana anavuja damu nyingi mdomoni baada ya mkewe kung'ata ulimi.

Mwanamke huyo alikamatwa baadaye na aliwaambia polisi kuwa hakuwa na furaha na maisha yake ya ndoa pamoja na muonekano wa mume wake usiovutia, na wakati wa majibizano alishindwa kuzuia hasira yake kabisa.
Na Mary Mkeu.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com au sms-whatsapp: +255765112259
VISA NA MIKASA: MWANAMKE MJA MZITO MBARONI KWA KUJARIBU KUNYOFOA ULIMI WA MUMEWE VISA NA MIKASA: MWANAMKE MJA MZITO MBARONI KWA KUJARIBU KUNYOFOA ULIMI WA MUMEWE Reviewed by By News Reporter on 10/01/2018 12:49:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.