Loading...

WEMA AMUANIKA LIVE MTARAJIWA WAKE

Loading...
Msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu ambaye wiki kadhaa alizindua filamu yake mpya ambayo amecheza na Staa wa Kimataifa wa Ghana, Van Vicker inayoitwa D. A. D (Day After Death), kufuatia kuwa na ukimya wa muda mrefu hatimaye amefunguka kuhusu mahusiano yake mapya.

Mrembo huyo ambaye ni pia ni Miss Tanzania 2006 ameweka wazi mahusiano yake kwa kumpost mpenzi wake huyo mpya kupitia ukurasa wake wa instagram na kuandika maneno yaliosomeka kwamba "my future husband" akimaanisha mume wake mtarajiwa.

Kwa kipindi kirefu kimwana huyo wa Bongo Movie amekua akificha mahusiano yake ya kimapenzi huku kukiwa na tetesi kama zote mtaani kuwa anajirusha na Supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye awali aliwahi kuwa mpenzi wake, lakini kitendo cha kumpost mpenzi wake huyo mpya kumefuta mzizi wa fitna kati yake na Diamond.
Na Geofrey Okechi.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WEMA AMUANIKA LIVE MTARAJIWA WAKE WEMA AMUANIKA LIVE MTARAJIWA WAKE Reviewed by By News Reporter on 10/18/2018 05:28:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.