Loading...

UHAKIKI MWINGINE VYETI FEKI WAJA

Loading...
SERIKALI imesema itafanya ukaguzi wa kushtukiza kwa baadhi ya taasisi na mashirika ya umma kutokana na baadhi ya waajiri kuwalinda ndugu na rafiki zao katika uhakiki uliopita wa watumishi hewa na wenye vyeti vya kughushi.

Vilevile, imesema imebaini idadi ya wanaolipwa mishahara ni kubwa kuliko waliohakikiwa kwenye taasisi hizo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema jana jijini hapa alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kikao kazi cha wakuu wa idara za utawala na rasilimali watu wa mikoa, idara, wizara, taasisi za umma na serikali za mitaa nchini.

Alisema hatua hiyo inalenga kujiridhisha kuhusu mafanikio ya uhakiki wa watumishi hewa na vyeti feki baada ya kubaini idadi kubwa ya watu wanaolipwa mishahara na serikali kulinganisha na idadi ya watumishi waliohakikiwa.

Uhakiki wa vyeti vya elimu na utaalamu wa watumishi wa umma ulianza Oktoba 2016. Uhakiki huo ulifanyika kutokana na ripoti mbalimbali za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kubaini serikali kulipa mabilioni ya shilingi kwa watumishi hewa na wasiokuwa na sifa.
Na Hamisi Chande.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UHAKIKI MWINGINE VYETI FEKI WAJA UHAKIKI MWINGINE VYETI FEKI WAJA Reviewed by By News Reporter on 10/18/2018 05:44:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.