Loading...
Jina TAIFA STARS lilianzishwa ghafla mno mwaka 1973 (miaka 45 na miezi michache iliyopita). Lilianzishwa bila mchakato wowote wa mapendekezo, mchujo wa mapendekezo wala kikao cha kupitisha jina hilo. Zaidi ya yote lilitoka ghafla kichwani mwa Mtanzania mwezetu mmoja huko Lagos Nigeria.
Ilikuwa hivi; mwaka huo, wanamichezo wetu walienda Nigeria kushiriki mashindano ya michezo mingi yaliyoitwa "All African Games". Hayo ni moja ya mashindano ambayo Tanzania ilifanikiwa sana. Kwenye riadha, Filbert Bayi alishinda mbio za meta 1500 kumshinda mwanariadha wa Kenya aliyekuwa hashindiki, Kipchoge Keino.
Kwenye soka, timu yetu ya taifa ilitoa wachezaji wawili kwenye 'kombaini' ya Afrika; kipa Omar Mahadhi bin Jabir toka African Sports ya Tanga na Maulid Dilunga toka Yanga. Cha kusisimua ni kwamba timu hiyo ilipoenda Mexico kushindana na timu za mabara mengine, MAHADHI NA DILUNGA WETU WALIPATA NAFASI YA KUCHEZA!
Sasa tuje kwenye jina TAIFA STARS. Timu za taifa za soka zilipokuwa zikiorodheshwa kwa taratibu mbali mbali za kimashindano hapo Lagos, Nigeria zilikuwa zinatakiwa kutaja majina ya timu hizo. Kwa mfano;Kenya? Harambee Stars, Uganda? Uganda Cranes. Nigeria? Green Eagles (enzi hizo). Ikaja zamu yetu sasa, kimbembe, timu ilikuwa haina jina. Tanzania? Ghafla tu kocha Mtanzania wa timu hiyo, Paul West Gwivaha (kwa sasa ni marehemu) akatamka " "TAIFA STARS". Ndivyo jina hilo lilivyoanza na kuwa sehemu ya taifa letu mpaka leo.
Gwivaha alituondolea fedheha kwani leo kina sisi tungejibu " kwa kweli hatujaipa jina timu yetu". Mtu akikuuliza bibi wa bibi yako mzaa mama aliitwa nani, taja jina lolote upate tiki. Kwani yeye anamjua?
Taarifa kama hizi zinafaa zitunzwe kwenye kumbukumbu rasmi ili uwepo utaratibu wa kuwaenzi walioanzisha mambo ya kudumu ya nchi kama Paul West Gwivaha na jina TAIFA STARS.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

ASILI YA JINA "TAIFA STARS"
Reviewed by By News Reporter
on
11/18/2018 11:06:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: