Loading...
Kabla haujafanya safari, zingatia mambo haya muhimu. Hiki ni kipindi ambapo wengi wanatarajia kupanda ndege kutoka eneo moja hadi jingine.
Kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wengi wanafikiria kwenda mapumzikoni kufurahia likizo baada ya kazi nyingi za kipindi cha mwaka mzima. Kabla haujafikiria ni raha za namna gani utakazokwenda kuzipata mji au nchi fulani, hakikisha unafanya vitu hivi vitano kwanza;-
i/. Chagua mahali pakupumzikia - Jiulize wapi hasa unataka kwenda? Kuna baadhi ya watu unakuta wanasafiri sehemu ambazo hawakuwa na malengo nazo huko nyuma. Kwa sababu tu, marafiki wamesema wanaenda Misri na wewe unaenda. Hapana hakikisha hiyo sehemu unayoenda ni sahihi kwako.
ii/. Fanya tafiti - Ushachagua mahali pakupumzikia sasa kinachofuata ni utafiti wa ndege zenye bei nafuu, hoteli utakazofikia, hali ya hewa ya huko kipindi hiki, hali ya usafiri wa sehemu hiyo, vyakula vinavyopatikana huko na usalama wa nchi/mji huo kimataifa.
iii/. Panga bajeti - Hakikisha unatenga bajeti fulani na uiheshimu ili usije ukajikuta unabaki miji ya watu kwa kukosa pesa.
iv/. Tunza nyaraka - Hakikisha unarekodi na kutunza nyaraka ya kila hatua ya safari kama bili zote, njia za safari, vituo vya mabasi, hoteli ulizofikia na maeneo uliyotembea ili iwafae wengine baadae.
v/. Wekeza - pesa utakazo tupia safari hakikisha unatafuta njia ya kuzirudishia kama zitakuwa zimetoka mfukoni mwako.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

NINI UNAPASWA KUJUA KABLA HAUJASAFIRI?
Reviewed by By News Reporter
on
11/18/2018 11:41:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: