Loading...
Mzee Nassir Abdi, 75, kutoka eneo la Old Town alisimulia wachawi hao wanaojulikana kama wanga hujigeuza na kuwa wanyama kama vile paka, panya na hata mbwa na kisha kuingia ndani ya nyumba na kumhangaisha mwenye nyumba.
Anaeleza kuwa jina paka mwanga lina chimbuko lake katika wachawi wengi waliojigeuza paka.
"Watu wakimgundua paka kama huyo basi utasikia wakisema huyu si paka bali ni mwanga," alieleza mzee Abdi mwenye umri mwa miaka 75.
Yapata miezi mitatu iliyopita Mariam Hussein alihisi mtu akimvuta mkono wake wa kushoto.
"Sikuamini, niliamka huku nikijaribu niwezavyo kujiokoa kutoka kwa mshiko huo wa mkono wa binadamu," alisema Mariam.
Yapata miaka 9 iliyopita, kulitokea kisa cha kushangaza katika eneo la Bamburi ambapo mchawi aliyejigeuza mwanga alikwama ndani ya chungu kidogo nje ya nyumba.
Inadaiwa mchawi huyo wa kike alikuwa amewahangaisha wapangaji kwa siku nyingi na hivyo mmoja wao akaamua kumwekea mtego al maarufu tego.
Paka huyo aliachiliwa na aliyeweka tego hilo baada ya muda wa saa 18. Hii ni baada ya polisi na viongozi wa kisiasa kumrai aliyeweka tego kumwachilia paka huyo baada ya watu wengi kuanza kumiminika eneo hilo na hivyo kuhatarisha usalama.
"Nilijaribu kumtoa paka huyo lakini nikashangazwa kuwa mdomo wa chungu hicho ulikuwa mdogo mno na hata haungetoshea vidole vitatu ya mkono," alisema mzee Hamisi aliyeshuhudia kisa hicho.
"Paka huyo alipotelea makaburini pindi baada ya kuachiliwa," alisema Mzee Hamisi.
Mzee Makasi Righa ambaye ameishi eneo la Bamburi kwa zaidi ya miaka 19 alisimulia kuhusu rafiki yake kutoka eneo la Magharibi mwa Kenya ambaye pamoja na mkewe alipokea kichapo kutoka kwa watu asiowajua.
Hili lilijiri pindi tu baada ya panya kuingia kwa nyumba. " Ilimbidi ahame na hali hiyo ya kutandikwa viboko ikakoma," alisema Mzee Makasi.
Mzee Makasi anasema kuwa tatizo la watu kuhangaishwa na nguvu za giza limechangia pakubwa kufanya mamia ya nyumba katika Pwani ya Kenya kuogopwa.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

PAKA, PANYA NA MBWA TISHIO MJINI MOMBASA WAHUSISHWA NA UCHAWI NA MAJINI
Reviewed by GEOFREY MASHEL
on
11/19/2018 12:22:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: