Loading...

KAMPUNI YA MAGARI NISSAN NA MITSUBISHI HISA ZAPOROMOKA

Loading...
Hisa za kampuni za kutengeneza magari nchini Japan Nissan na Mitsubishi, zimeshuka baada kukamatwa kwa Mwenyekiti Carlos Ghosn kwa madai ya matumizi mabaya ya fedha.

Kukamatwa kwa Ghosn kumetikisa masoko ya biashara ya kampuni hizo ambazo zinatatengeza magari ya kuyauza duniani, hali ambayo pia imeathiri biashara katika masoko ya Tokyo.

Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hizo watakutana siku ya Alhamisi na kufikia uamuzi wa kumfuta kazi Bwana Ghosn ambaye sifa yake nzuri katika kampuni hiyo sasa, imepakwa tope kutokana na madai yanayomkabili.

Licha ya kukamatwa kwake, viongozi wa mashtaka nchini Japan hawajaeleza kwa kina kuhusu kukamatwa kwake, lakini ripoti zilizochapishwa kwenye Magazeti nchini humo zinaeleza kuwa, Ghosn alitumia vibaya zaidi ya Yen Bilioni tano kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Na Hamisi Omari.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KAMPUNI YA MAGARI NISSAN NA MITSUBISHI HISA ZAPOROMOKA KAMPUNI YA MAGARI NISSAN NA MITSUBISHI HISA ZAPOROMOKA Reviewed by By News Reporter on 11/20/2018 11:18:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.