Loading...

UTAFITI UNAONYESHA KUNYWA MAJI KUPITA KIASI KUNADHURU AFYA

Loading...
Matatizo yanayotokana na ukosefu wa maji ya kutosha mwilini ni wazi yanajulikana. Hata hivyo sasa wataalamu wanaonya kuwa unywaji wa maji kupita kiasi huenda ukamsababishia mtu matatizo ya kiafya na hata kusababisha kifo.

Mtu mzima anahitaji kati ya lita 2-4 za maji kila siku. Lakini pia inaelezwa kuwa mwili wa binadamu hauwezi kumudu mchakato wa matumizi ya zaidi ya lita moja ya maji kwa saa.

Hivyo, maji yanayobakia huhifadhiwa kwenye seli za mwili na kuzifanya kuvumbiwa. 

Kulingana na utafiti huo uliofanywa na Liz Weinandy, mtaalamu wa lishe katika Chuo Kikuu cha Ohio State University, uloweshaji wa seli za mwili na maji kupita kiasi husababisha kiwango cha madini ya natiri (sodium) kushuka na hivyo kuufanya mwili kuwa na kazi ngumu ya kudhibiti shinikizo la damu (presha).

Dalili za unywaji wa maji kupindukia ni pamoja na kuumwa na kichwa, kuchanganyikiwa, kujihisi mchovu kupindukia na shinikizo la damu.

Aidha, hali hiyo inaweza kuchangia mgonjwa kupoteza fahamu na hata kufa.

Madaktari huwataka watu kuangalia rangi ya mkojo ili kutambua iwapo mtu amekunywa maji kupita kiasi.
Na Richard Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UTAFITI UNAONYESHA KUNYWA MAJI KUPITA KIASI KUNADHURU AFYA UTAFITI UNAONYESHA KUNYWA MAJI KUPITA KIASI KUNADHURU AFYA Reviewed by By News Reporter on 11/21/2018 07:03:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.