Loading...
Maafisa watano wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC), wamefikishwa Alhamisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, Tanzania, wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali ya uhujumu uchumi.
Maafisa hao kwa majina ni Deusdedith Katwale (38), Lilian Laizer (27), Luciana Lawi (33), Edna Lutanjuka (51) na Mwaruka Miraji (42). Walifikishwa kizimbani siku ya Alhamisi.
Mbali na shtaka la kwanza ambapo washtakiwa hao wanadaiwa kuisababishia NEMC hasara ya Sh. milioni 160, mashtaka mengine yanayowakabili ni kula njama kutenda kosa la kughushi, kuwasilisha hati bandia na kusababisha hasara kwenye mamlaka husika.
Baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka yao, upande wa mashtaka uliomba kutoa hati ya kumkamata ofisa mwingine wa NEMC, Magori Wambura, ambaye anakabiliwa na mashtaka kama hayo. Mahakama iliridhia maombi hayo na kuamuru akamatwe.
Na Petro Bahati.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MAAFISA WATANO WA NEMC KORTINI KWA UHUJUMU UCHUMI
Reviewed by By News Reporter
on
11/02/2018 07:40:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: